Na Abdallah Amiri, Igunga
, amewaonya watendaji wa vijiji na kata kuacha tabia ya kuondoka katika vituo vyao vya kazi, hali inayosababisha usumbufu kwa wananchi.
Hayo aliyasema jana mjini hapa, katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Ntobo, wakati alipokuwa kwenye mwendelezo wa ziara zake za kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Kutokana na tabia hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alisema anachukizwa na uongozi wa Kijiji cha Ntobo kwa kushindwa kuwahamasisha wananchi shughuli za maendeleo katika eneo lao.
Hata hivyo, pamoja na Mkuu wa Wilaya kukaa kwa muda wa saa moja, wananchi waliokuwa wameongezeka katika mkutano huo walikuwa 23 na kufanya idadi kufika watu 30, ndipo mkuu huyo alipomwagiza mwenyekiti wa kijiji hicho kufungua mkutano huo.
Alisema kwa uchungu huku akitoa ujumbe mzito kwa viongozi wote wa vijiji na kata ambapo alimwagiza Ofisa Mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji kuitisha mkutano mwingine.