30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

DC Hapi atoa siku 14 kwa uongozi wa Soko la Magomeni kuondoa baa na ghala.

NA CHRISTINA GALUHANGA

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa siku 14  kwa uongozi wa soko la Magomeni kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo katikati ya soko hilo.

Akizungumza katika ziara yake ya siku 10 ndani ya wilaya hiyo, Hapi alisema inasikitisha.kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.

Alisema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inasababisha kuwanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wale wadogo.

"Ninatoa siku 14 kwa viongozi wa.soko na.manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa wenzao hapa hapawafai," alisema Hapi.

Sambamba na hilo mkuu huyo America siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya soko.

Alisema sheria zipo wazi na hakuna aliyejuu ya sheria zaidi ya kuzingatia sheria hizo.

"Hakuna aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanyabiashara nje ya soko hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko," alisema Hapi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles