22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

DC HAPI AMSIMAMISHA KAZI MWANASHERIA

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amemsimamisha kazi kwa muda mwanasheria wa manispaa hiyo, Arnod Kinyaia, kwa tuhuma za kuwakumbatia matajiri ambao wanawanyanyasa wananchi wenye kipato cha chini.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kinondoni katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi, Hapi alisema watendaji wengi wamekuwa na mchezo wa kuwakumbatia matajiri, huku wakichangia kupoteza haki za wanyonge.

Alisema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wa Kampuni ya uzoaji taka ya Total West Solution, ambapo wafanyakazi hao 13 walifanya kazi kwa muda wa miaka mitatu na kufukuzwa bila kupewa mshahara wao nusu waliokuwa wakiudai kwa miaka hiyo.

Hapi alisema anafahamu kuna malalamiko ya ulaji rushwa kwa baadhi ya watendaji, jambo ambalo limekuwa likiichafua wilaya hiyo.

“Ninafahamu kuna fununu za ulaji rushwa ambao umekuwa ukichangia watu kupoteza haki zao, huku watendaji hao wakijinufaisha kwa matajiri hao,” alisema Hapi.

Alisema kamwe hatachoka kuwafukuza kazi watendaji wanaokiuka maagizo yake na kujinufaisha kwa matajiri wachache.

Kwa upande wake, Ridhiwan Husein  ambaye alikuwa dereva katika kampuni hiyo, alisema walipeleka malalamiko yao ya kutolipwa fedha kwa Mkuu wa Wilaya ambaye aliwapeleka kwa Mwanasheria wa Manispaa na kufahamu kiasi wanachodai.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles