27.8 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

DC awataka wananchi kutotumia mifuko ya ‘rambo’

Na Elizabeth Kilindi-Njombe

MKUU wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, Ally Kassinge, amewataka wananchi wilayani humo kuacha kutumia mifuko ya plastiki maarufu ‘rambo’, badala yake watumie mifuko ya karatasi ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

Wito huo ameutoa mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa kampeni wa usafi mjini Igwachanya, wilayani humo ambapo alisema mifuko ya rambo imekuwa moja ya chanzo cha kuchafua mazingira kutokana na kwamba zikiisha matumizi zinatupwa na kusambaa katika maeneo mbalimbali.

“Tatizo la rambo ukishatumia inaisha matumizi badala yake mnazitupa tu na zenyewe zinapeperuka katika maeneo mbalimbali na kuchafua mji wetu,” alisema Kassinge.

“Uchafu mkubwa unaozalishwa hapa Igwachanya ni maganda ya miwa, makopo pamoja na mifuko ya rambo kupitia kampeni hii ya usafi tuliyozindua, nasema hivi mifuko ya rambo kwa sababu bado ipo katika mzunguko madukani na ifikapo Desemba 31, mifuko ya rambo marufuku Igwachanya,” alisema Kassinge.

Aidha, Mkuu wa wilaya huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka watendaji katika halmashauri hiyo kusimamia jambo hilo ili kuweza kuleta tija.

“Jambo hili kwa sasa nalikabidhi kwa watendaji wenzangu ngazi ya kata na kijiji, eneo langu la kufanyia kazi inatosha na wakishindwa mimi nitaanza kufanya kazi na wao,” Kassinge alisema.

Kwa upande wa mkazi wa mji wa Igwachanya, Mary Wiheuri, alimshukuru mkuu wa wilaya na kwamba, ‘rambo’ ni chanzo kikuu cha uchafu na zikidhibitiwa itasaidia kufanya mji huo kuwa safi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,383FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles