23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

DC atoa mwezi mmoja wananchi kujenga vyoo 608

Na Ibrahim Yassin,Songwe

MKUU wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Irando amewataka wananchi waishio kwenye kaya 608 ambazo zimebainika kutokuwa na vyoo wawe wamejenga na kuvikamilisha mwezi machi mwaka huu vinginevyo amesema zitageuka kuwa vyanzo vya mapato.

Wilaya ya Momba yenye majimbo mawili,ina kaya 76,121, kati ya hizo,608 hazina vyoo hali iliyopelekea mkuu wa wilaya hiyo kuzitaka mamlaka husika wakiwemo maafisa afya,watendaji na viongozi wengine kuhakikisha kaya hizo zinajenga vyoo nani ya miezi miwili.

Awali akisoma taarifa ya hali ya usafi wa mazingira katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na bingwa wa mashairi nchini Mrisho Mpoto wakati wa majumuisho ya utoaji hamasa,afisa afya wa halmashauri ya mji wa Tunduma,Sayune Mwasha alisema kaya zisizo na vyoo ni 71.

Alisema baada ya kutolewa kampeni hiyo,wao walianza kutoa elimu kwa kila kijiji ambapo wananchi walihamasika ambapo wengine walijenga vyoo na wengine waliviboresha vilivyokuwa vibovu na kwamba anashangaa kuona kaya 71 kati ya 39,902 za Tunduma hazina vyoo.

Ofisa Afya Wilaya ya Momba,Naye Mary Swilla lisema halmashauri yake ina kaya 36,219 kati ya hizo,537 hazina vyoo na kwamba licha ya kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara bado kaya hizo hazijajenga na kuwa wameweka mikakati kuhakikisha vyoo vinajengwa.

Mkazi wa Tunduma, Martin Mboya  alisema anashangazwa na taarifa hiyo,akisema kuwa mji huo wenye utajiri na fursa nyingi za kibiashara,hivyo kitendo cha kaya 71 kutokuwa na vyoo ni aibu,amevitaka vyombo husika kushughulika na watu wa kaya hizo ili zijenge vyoo.

Baada ya mazungumzo hayo ya wananchi,muendeshaji wa kampeni ya ujenzi wa vyoo bora nchini,Mrisho Mpoto,alisema alipoingia na kufanya hamasa katika wilaya hiyo,alitegemea atakuta kila kaya ina choo bora lakini imekuwa tofauti hivyo alitaka kujua ni lini kaya hizo zitakamirisha ujezi.

”Nimezunguka kata mbalimbali katika wilaya hii,nimekuta baadhi ya watu hasa jamii ya wafugaji wanajenga vyoo kwa ajili ya wageni,wao wakiendelea kujisaidia vichakani wengine kwenye mashaba ya mahindi wakidai kuwa wamerithi kutoka kwa babu zao”alisema Mpoto.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Ally Mwafoingo na makamu wake, Yerode Jivava kwa nyakati tofauti wameonyesha kuchukizwa na takwimu hizo ambao wameahidi kuwa kila diwani ambaye kwenye maeneo yake kutoakuwa na kaya hazina vyoo kuhakikisha zinajengwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles