21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

DC atangaza vita watumiaji dawa za kulevya Tanga

Oscar Assenga -Tanga

MKUU wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, ametangaza vita mpya kwa watumiaji wa dawa za kulevya huku akiwataka wazazi wenye watoto wanaojihusisha na utumiaji wa dawa hizo wawaonye.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa watumiaji wakubwa wa dawa za kulevya wapo Kata ya Majengo jijini Tanga, huku eneo ambalo limekuwa ni sugu ni kuanzia barabara 13 hadi 18.

Akizungumza wakati akihamasisha ujenzi wa vyumba vya madarasa Jiji la Tanga, Mwilapwa alisema jiji la Tanga ni la pili kwa matumizi na uuzaji wa dawa  za kulevya baada ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, alisema hivi sasa wamejipanga imara kuweza kukabiliana na suala hilo, hasa kwenye eneo la Majengo ambalo limeshamiri kwa matumizi hayo.

“Siku mbili kabla ya Sikukuu ya Krismasi mwaka jana nilikwenda kuitisha mkutano na wananchi wa eneo hilo na kukiri hali sio nzuri, na niliwaeleza wazazi kwamba kama wana watoto wanaotumia dawa hizo wawaonye,” alisema Mwilapwa.

Alisema kwamba alifika Kata ya Majengo na kukutana na wananchi hao lengo kubwa likiwa ni kufikisha ujumbe waachane na matumizi ya dawa za kulevya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,590FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles