23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC atangaza kuwapeleka gerezani wazazi wasiopeleka watoto shule

Derick Milton -Bariadi

MKUU wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Festo Kiswaga, ametanga opereisheni itakayoanza kesho ya kukamata wazazi ambao hajawapeleka watoto wao waliofaulu kuanza kidato cha kwanza na kwamba watakaokamatwa watapelekwa gerezani moja kwa moja.

Alitoa tangazo hilo hivi karibuni wakati akizungumza na wazazi, walimu, viongozi na wadau wengine wa elimu wilayani humo wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi na walimu waliofanya vizuri kwenye mitihani ya taifa 2019.

Alisema bado kuna idadi kubwa ya wanafunzi katika Wilaya hiyo haswa Bariadi Vijijini ambao hawajapelekwa shule licha ya kufaulu kwensa sekondari.

Aliwataka wazazi ambao hawajafanya hivyo na wanajua wana watoto waliofahulu kwenda kidato cha kwanza, wajiandae kwa ajili ya kupelewa gereza la Maswina lililoko wilayani humo.

“ Natagaza kuwa opereisheni itaanza Februari 3, siku ya Jumatatu, kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mimi tutafanya opereisheni hiyo, kama haujapeleka mtoto shule sehemu yako salama ni gereza la Maswina.

“Wazazi ambao mnajua bado hamjafanya hivyo, siku hiyo tafuteni nguo nzuri mkavae kwa ajili ya kwenda gerezani, hatutakuwa na mzaha kwenye hili, Rais ametoa elimu bure lakini mpaka leo kuna watu hawajapeleka watoto shule,” alisema Kiswaga.

Ofisa Elimu Sekondari halmashuari hiyo, Hamis Shololo, alisema wanafunzi 1,120 kati ya 4,188 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2020, hajaripoti shuleni hadi sasa.

Akizungumzia hali ya ufahulu Mkuu huyo wa Wilaya alisema halmashuari hiyo imefanya vizuri kwenye mitihani ya shule za msingi, lakini sekondari bado kwani imekuwa ya tano kati ya halmashuari sita.

“Tumeweka mikakati kubwa eneo la sekondari ambalo bado tuko nyuma, tuongeze ushirikiano zaidi kwa wadau wote na walimu kuhakikisha wanatimiza wajibu wao,” alisema Kiswaga.

Aliwataka walimu wakuu kupunguza migogoro na walimu wenzao, huku akitaka ofisi zote za umma kwenye halmashuari hiyo kuhakikisha wanawapa kipaumbele cha kwanza walimu katika kuwapa huduma.

Awali Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, James John, alisema idara ya elimu sekondari, imejipanga kwa kiwango kikubwa kuhakikisha wanaongeza ufahulu mwaka huu.

John alisema idara hiyo itatoa zawadi kwa walimu kama motisha ambao wanafunzi watafanya vizuri zaidi kwenye masomo yao, jambo alilosema litapaisha hali ya ufundishaji kwenye halmashuari hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles