23.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

DC APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUJIPIKIA CHAKULA

NA  FRANCIS GODWIN- IRINGA

MKUU  wa  Wilaya ya Kilolo  mkoani  Iringa, Asia Abdalah, amepiga marufuku wanafunzi  wa shule za msingi  wilayani  humo  kujipikia chakula wakati  wa masomo .

Alikuwa akizungumza  jana  na walimu   na kamati ya  Shule ya Msingi Mlowa Kata ya Mahenge  wakati wa ziara  yake ya kukagua miundombinu ya  shule.

Alisema     hajapendezwa na utaratibu wa  shule  hiyo wa  kuwaacha  wanafunzi  kuingia  jikoni  kujiandalia  chakula cha  mchana badala ya  kujisomea.

DC aliagiza kamati ya  shule  hiyo na  shule  nyingine  zote  wilayani  Kilolo  kutafuta  wapishi  watakaofanya kazi ya  kuwaandalia  chakula   wanafunzi hao.

Alisisitiza kuwa  asingependa  kuona  wanafunzi  wakiacha masomo na kuingia  jikoni  kupika  chakula.

 "Sijapendezwa  hata  kidogo  kuona  wanafunzi  wanapika chakula badala ya  kusoma, naagiza kuanzia leo shule  zote  kutafuta  wapishi  wa  kuwahudumia  wanafunzi hao.

“Sitegemei  kuona  tena  wanafunzi  wanajipikia chakula….natoa  muda  hadi Jumatatu wiki ijayo iwe  mwisho,”alisema.

Hata hivyo, DC  alipongeza  jitihada mbalimbali  zinazofanywa na kamati ya  shule hiyo  kwa kukamilisha vyumba  viwili   vya madarasa na  kuwaepusha  wanafunzi  waliokuwa  wakisomea  chini ya  mti  kuanza  kusomea darasani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,293FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles