24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

DC amtimua mkandarasi wa barabara

Walter Mguluchuma  -Katavi

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi, Salehe Mhando amemfukuza kufanya kazi ya kutengeneza barabara mkandarasi wa Kampuni ya LGNA ya mkoani Tabora, Michael Kessy.

Kutokana na hilo, ameagiza Taasisi na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuchunguza namna mkandarasi huyo alivyopewa kazi ya kutengeneza barabara ya Kijiji cha Mnyagala yenye urefu wa kilomota 1.5 kwa kiwango cha changalawe baada ya kushindwa kuikamilisha.

Alitoa agizo hiyo jana mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo inayotengenezwa na mkandarasi huyo, ambayo inatengenezwa kwa gharama ya Sh milioni 74.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo kama fedha za kwenye barabara hiyo, lakini aina ya wakandarasi wanaopewa kazi hawafai.

“Kuanzia sasa sitaki kumwona mkandarasi huyu kwenye barabara hii na kwenye wilaya yangu na akiletwa mkandarasi yeyote feki nitahakikisha ninamnyoosha.

“Pia naagiza Takukuru kumfuatilia mkandarasi huyo kama kweli anazo zifa zilizomfanya apewe kazi na kama ana sifa ya kufanya kazi ya ukandarasi na jinsi mchakato wa kumpa kazi ulivyofanyika na bodi ya manunuzi,”alisema.

Kaimu Meneja wa Tarura wa Halmashauri ya Tanganyika, Mwandisi Mkila Richald alieleza kuwa mradi huo ulianza Novemba mwaka jana na unatakiwa kukamilika Aprili 6 mwaka huu na hadi sasa matengenezo ya barabara hiyo yamefikia asilimia 10 tu.

Alieleza tayari wameshamwandikia barua tatu mkandarasi huyo za kumtaka atekeleze kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba wake unavyoeleza.

Diwani wa Kata ya Mnyagala, Mathias Nyanda alieleza kuwa kutokamilika kwa barabara hiyo imekuwa ni changamoto kubwa na hasa mtu anapokuwa ameugua, wamekuwa wakisafirishwa kwa shida kubwa hadi kufikishwa katika Hospitali ya Mpanda Mjini wanakopatia huduma .

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles