27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DC alia na wazazi kukwamisha kesi mimba za wanafunzi

Na DERICK MILTON

MKUU wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera amesema   wazazi na walezi wa wanafunzi wanaopata mimba, wamekuwa kikwazo kikubwa kushindwa kuendelea kwa kesi za watu wanaotuhumiwa kuwapa ujauzito.

Mwera amesema   wazazi wamekuwa wakiwatorosha watoto wao   watuhumiwa wanaowapa ujauzito huo wanapofikishwa mahakamani  ambako wengi hudai  watoto wao wametoroka jambo ambalo sio kweli.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa hadi kufikia  Machi  mwaka huu wanafunzi 53 wa kike, shule za msingi 17 na sekondari 36 walikutwa na ujauzito wakiwa shuleni.

Alisema  kesi nyingi za wanafunzi hao 53 zilipelekwa mahakamani, lakini mpaka leo hakuna kesi hata moja ambayo ambayo imetolewa hukumu kutokana na nyingi kuishia njiani.

“Kesi zimekuwa zikivunjika, hazifiki mwisho, watuhumiwa na wazazi/walezi wa wanafunzi hao wamekuwa wakielewana nje ya mahakama na kuamua kutofika mahakamani,” alieleza Mwera.

“Unajua Mwanafunzi wa kike aliyepewa mimba ni shahidi namba moja na muhimu mahakamani, akikosa huyo kesi haiendelei tenana wazazi wamekuwa wakiwatorosha, tatizo hawana elimu ya kutosha na umaskini ndiyo unachangia sana,” anaeleza Mwera.

Alisema   aliamua kuanzisha kampeni ya Paza Sauti inayolenga kupiga vita mimba za utotoni na ndoa za utotoni ambako anashirikiana na shirika la Amref Health Africa.

Mwera alisema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wanafunzi wa kike shule za msingi na sekondari  na wanaelimishwa kujitambua, kujithamini, pamoja na kutambua umihimu wa elimu katika maisha yao.

“Kampeini hii ilianza mwezi Machi mwaka huu, nashirikiana na Amref ambako tunawafikia wanafunzi kwa kuwaelimisha wajitambue, wajithamini.

“Pia tunawaelimisha wazazi umuhimu wa kutoa ushirikiano mahakamani,” alisema.

DC alisema kwa kushirikiana na mradi wa Amref wa Uzazi Uzima  unaofadhiliwa na serikali ya Canada unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoani Simiyu, wamepanga kuwafikia wanafunzi wote na kutoa elimu kwa wananchi kwenye mikutano ya hadhara.

Hadi sasa mradi wa Uzazi Uzima umetoa elimu kwa walimu wa shule takribani 145 za Mkoa wa Simiyu kuhusiana na afya ya uzazi, jinsi ya kuepuka mimba za utotoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles