29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

DC AKATAA MAABARA YA SHULE KUZINDULIWA NA MWENGE

 

                                                                 |Mohamed Hamad, Manyara


Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino  Mofuga, amekataa mradi wa jengo la Maabara la Shule ya Sekondari Labay kuwapo katika miradi itakayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Aidha, Mofuga amemtaka Mhandisi wa wilaya hiyo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu sababu ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango pamoja na gharama zilizotumika.

Mofuga ameukataa mradi huo akiwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotarajiwa kuzinduliwa na mwenge mwaka huu na kuongeza kuwa hatakuwa tayari kuupeleka mwenge katika miradi ambayo ubora wake unatia mashaka ikiwepo jengo hilo ambalo matofali yake hayajakidhi ubora unaotakiwa.

“Nimeangalia baadhi ya miradi lakini hairidhishi, naagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa kumtumia mhandisi wake kutoa elimu hasa ya ubora wa majengo kuchunguza ubora wa  jengo hili kisha kuniletea taarifa sahihi za sababu ya mradi huo kujengwa chini ya kiwango,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles