27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

DC AGIZA OFISA ARDHI AWEKE LUPANGO

NA CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM


MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ameagiza Jeshi la Polisi kumuweka mahabusu Ofisa Mthamini Ardhi wa wilaya hiyo, Einhard Chidaga baada ya kukacha ziara yake kwa siku tano mfululizo.

Hapi alitoa agizo hilo baada ya wananchi wa Kata ya Wazo wilayani humo kulalamikia usumbufu wanaoupata katika Kitengo cha Ardhi   wanapoomba kupimiwa na kuthaminishiwa maeneo yao.

“Haiwezekani kila siku hapa mthamini anatafutwa ajibu maswali haonekani,  naagiza polisi mtafuteni popote alipo na awekwe mahabusu kwa  saa 48,” alisema Hapi.

Katika mkutano huo, wananchi walikuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakilalamikia  viongozi na watendaji wa Mtaa wa Kilimahewa wakimtaka mkuu huyo wa wilaya kuwaondoa kwa sababu wamekuwa wakikwamisha maendeleo ya mtaa wao.

Wakati huohuo, Hapi amepiga marufuku kuendesha mnada katika uwanja wa kwa Mkanada kwa sababu  eneo hilo limepita bomba kubwa la maji.

Vilevile,  amepiga marufuku wenyeviti wa mitaa kutoza fedha kwa ajili ya huduma mbalimbali za  jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles