23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

DC aeleza sababu polisi kuzingira mkutano wa Mbowe

OMARY MLEKWA -HAI

MKUU wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya, amesema kuwa amelazimika kupeleka polisi katika mkutano wa Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ambaye alikuwa akizungumza na wanachama wa Chadema wilayani hapa.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa kuwapo polisi ni jambo la kawaida kwani huo si mkutano wa ‘send off’ bali ni wa chama cha siasa ambapo jambo kama hilo pia hufanywa hata kwa CCM.

Kauli hiyo aliitoa baada ya tukio la jana ambapo Freeman Mbowe na wenzake, walijikuta wakifanya mkutano wa ndani huku wakiwa wamezingirwa na polisi.

Polisi hao wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Lwelwe Mpinga, walifika ofisi za chama hicho zilizopo Mtaa wa Gezaulole, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wakiwa wamejizatiti.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, alisema alipata taarifa ya kufanyika kikao hicho na kuamua kupeleka askari ili kuhakikishia usalama wao na wajumbe wote waliopo unaimarishwa.

“Kwa kuwa ni kikao cha chama cha siasa na sio kikao cha harusi, kama mijadala yao haina tatizo, Serikali ina haki za kutuma vyombo vya dola kwa ajili ya usalama wao na usalama wa wengine.

“Hata mikutano ya vyama vingine vya siasa kama CCM, polisi huwa wanakuwa ndani kwa ajili ya usalama, kama wewe sio mhalifu una haja gani ya kuogopa askari?

“Baada ya kuona ni kikao cha ndani, tuliona polisi wakae wasikilize, maana desturi yao na rekodi yao huwa inaonyesha mijadala, siasa zao zimekuwa zikigawa watu, polisi watawasaidia kuweka maelezo na mstari utakaowasaidia kuepuka kupelekana mahakamani eti kwa sababu ya siasa za uchochezi na kugawa watu.

“Endapo kikao hicho kitaonekana kuvunjiana  heshima kwa vyama vingine vya siasa, kutumia lugha zisizo na heshima, polisi watasaidia ili kuepuka kukimbizana, nataka kuanzia mwanzo kuzuia yasitokee na kwa kuwa ni mkutano wa ndani hakuna haja ya kuvunjiwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles