23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

D’BANJ: NIMEFUNGA NDOA NA MUZIKI

LAGOS, NIGERIA


MKALI wa muziki nchini Nigeria, Oladapo Oyebanjo maarufu kwa jina la D’banj, ameweka wazi kuwa bado ana deni kubwa kwenye muziki kwa kuwa amefunga ndoa na kazi hiyo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 37, alifunga ndoa na mpenzi wake, Lineo Kilgrow, tangu mwaka 2016, lakini amedai kufunga ndoa ya kudumu na muziki.

“Naweza kusema nina deni kubwa katika muziki, ili niweze kulilipa lazima nihakikishe ninaendelea kufanya vizuri kwa kipindi kirefu.

“Nyimbo zangu zote ni bora japokuwa kwa sasa ninafanya vizuri na wimbo wa ‘Tongolo na Suddenly’, lakini ukweli ni kwamba nyimbo zangu zote ni bora kwa kuwa nimeamua kufunga ndoa ya kudumu na muziki,” alisema D’banj.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles