30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Dawasa yatoa ajira 105 kwa vijana

RAHMA SWAI (TSJ) na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAMMamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imetoa ajira kwa vijana 105 waliohitimu Chuo cha Mafunzo stadi (Veta) kusaidia kusambaza maji katika miradi mipya.

Akizungumza katika ziara ya Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa aliyoifanya katika eneo la Salasala, kata ya Wazo manispaa ya Kinondoni jijini hapa,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema vijana hao wameanza kazi rasmi jana.

“Tumetoa ajira ya muda kwa vijana 105 kutoka Chuo cha VETA ambao wameanza kazi rasmi leo ambao watakuja hapa na kufanya maunganisho kwa wakazi,” amesema Luhemeja.

Kwa upande wake Profesa Mbarawa ameitaka Dawasa kuharakisha kuwapatia maji wakazi hao kwa kuwa mradi huo tayari umekamilika.

“Tulikubaliana katika vikao mtoe ajira kwa vijana wa Veta kurahisisha usambazaji wa maji kwa wananchi, mpaka sasa naona kimya leteni vijana 50 katika eneo hili” amesema

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles