24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dawasa yaongeza makusanyo kutoka bilioni 2.9 kwa mwezi hadi bilioni 10.5

TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM



Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), imeongeza makusanyo ya maduhuli yake kutoka Sh bilioni 2.9 kwa mwezi mwaka wa fedha 2014/15 hadi kufikia Sh bilioni 10.5 kwa mwezi katika mwaka wa fedha 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam leo Novemba 16, 2018 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema lengo ni kufikia Sh Bilioni 12.
Amesema mafanikio hayo yamekuja kutokana na ufanisi wa miradi mbalimbali iliyosababisha kuongezeka kwa maji yanayozalishwa pamoja na kuimarika kwa mfumo wa utendaji kazi wa Dawasa.

“Mafanikio haya yanatokana pia na usimamizi wa utoaji huduma na ukusanyaji mapato yatokanayo na uuzaji wa maji safi na maji taka katika eneo la huduma,” amesema Luhemeja.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano, miradi mikubwa iliyokamilika ambayo ni pamoja na upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu na chini ambao umesaidia kuongeza wingi wa maji hadi kufikia lita Milioni 502 kwa siku.

“Tumeweza kulaza mabomba yenye urefu wa kilomita 500 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuweza kugawa maji kwa uwiano mzuri zaidi na kuifanya mamlaka kuwa na mtandao wa kilomita 3,000,” amesema Luhemeja.

Amesema pia mamlaka hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa mradi wa uchakataji majitaka katika eneo la jangwani huku miradi mingine midogomidogo 50 itajengwa.
“Miradimikubwa mitatu ya kuchakata majitaka inatarajiwa kuanza hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kufikisha asilimia 30 ya huduma ya uondoshaji majitaka,” amesema Luhemeja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles