24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Dawasa kutoa leseni kwa wamiliki wa visima vya maji

Tunu Nassor-Dar es Salaam

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (Dawasa) imewataka wamiliki na wasambazaji wa maji ya kisima kujitokeza ili wapewe leseni na cheti cha kusambaza baada ya kupimiwa ubora wake.

Akizungumza katika ziara aliyoifanya kutembelea miradi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo leo Aprili 9, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa mhandisi Cyprian Luhemeja amesema lengo ni kuhakikisha maji yanayotumiwa na wakazi wa eneo la huduma yanakuwa safi na salama.

Amesema kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi kusambaza maji katika eneo la huduma la mamlaka hiyo bila kuwa na leseni.

“Tumeanza kuvitambua visima vyote vinavyotoa huduma ya maji na kupima maji yake bure ili wakazi wapate maji safi na salama,” amesema Luhemeja.

Amesema kwa sasa watu 10700 wanatumia  maji ya visima na kwa kupima maji yake itasaidia kuondoa kabisa changamoto ya magonjwa ya mlipuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles