24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

DAWASA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KWA SIKU SABA MFULULIZO

Tunu Nassor, Dar es Salaam

KUELEKEA kilele cha wiki ya Maji Machi 22, Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imesogea karibu na wananchi kwa kufungua dawati maalumu la kusikiliza wateja wake kwa muda wa siku saba.

Dawati hilo litakuwa katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa siku zote hizo kuanzia leo Machi 16, 2019 hadi Machi 22 mwaka huu.

Ofisa Habari Mwandamizi wa Dawasa, Everlasting Lyaro amesema wataalamu wa maji kutoka Dawasa na halmashauri zote za jiji watakuwapo katika dawati hilo. 

“Lengo ni kuwezesha wananchi kupata majibu ya kina ya changamoto zinazohusu  majisafi na majitaka,” amesema Everlasting.

Amesema itakuwa fursa kwa wananchi kupata maelezo ya mipango inayoendelea kutekelezwa ili kuboresha sekta ya maji katika jiji la Dar es Salaam na miji ya mkoa wa Pwani.

Everlasting amewataka wakazi wa jiji hilo wajitokeze kutoa kero zao kwa maana zitafanyiwa kazi na kutatuliwa ndani ya saa 24.

Kaulimbiu katika wiki hii ya maji ni ‘Hakuna atakayeachwa, kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira kwa dunia inayobadilika,”  amesema Everlasting.

Kwa upande wake, Mmoja wa wateja waliofika kuhudumiwa, Sheilla Mushi amesifu mabadiliko na ubora wa huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

“Siku hizi wamerahisisha kupata huduma hata kama hujapata ankara yako ya mwezi unaweza kutumia simu ya mkononi ukaipata,” amesema Sheilla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles