31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Dawasa kusambaza maji kutoka Kisarawe hadi Dar


 Tunu Nassor, Dar es Salaam 

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (Dawasa) imeanza ujenzi wa mradi wa usambazaji maji safi kutoka tenki la Kisarawe hadi Ukonga.

Akizungumza katika ziara aliyoifanya jijini hapa leo Aprili 11, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huo ni moja kati ya mikakati waliyojiwekea kupeleka maji katika maeneo ya pembezoni mwa jiji.

Amesema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi nane ambapo utakamilika Desemba Mwaka huu.

“Tumeanza ujenzi wa kutoa maji katika tenki la Kisarawe na kuleta Dar es Salaam ya kusini ambapo mradi huu utawanufaisha wakazi wa Majohe, Pugu, Chanika, Gongolamboto na Ukonga,”amesema Luhemeja.

Amesisitiza kuwa vifaa na fedha za mradi huo zipo na tayari mkandarasi ameshaanza kazi.

Aidha Luhemeja ameanza ziara ya kutembelea miradi 41 inayotekelezwa na Dawasa ikiwa ni miezi sita tangu kuunganishwa kwa Dawasa na lililokuwa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (Dawasco).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles