24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Dawa za kulevya zampeleka jela miaka 30

Na KULWA MZEE

DAR ES SAALAM

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi, maarufu ‘Mahakama ya Mafisadi’ imemtia hatiani na kumuhukumu raia wa Nigeria, Christian Ugbechi (28) kwenda jela  miaka 30 kwa kosa la  kusafirisha pipi 56 za dawa za kulevya aina ya heroin hydrochloride.

Hukumu hiyo ilitolewa jana mbele ya Jaji Sirrilius Matupa baada ya Mahakama kuridhishwa kwamba upande wa mashtaka  umeweza kuthibitisha kosa pasipo kuacha shaka.

Alisema ili kuthibitisha makosa hayo upande wa mashtaka uliita mashahidi wake 11 waliofika mahakamani na vielelezo 22.

Mahakama hiyo imeamuru dawa za kulevya alizokutwa nazo mshtakiwa ziteketezwe kwa mujibu wa sheria.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Matupa alisema mahakama imemuhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani na si kifungo cha maisha  kwa sababu imeona inayo mamlaka ya kumpa mshtakiwa adhabu kwa jinsi yenyewe inavyoona kutokana na mkanganyiko uliopo kwenye kifungu cha sheria cha 15(1)(a) na 15(1).

“Sheria hizo mbili zilikuwa na madhumuni tofauti kutokana na matumizi ya maneno hayo shall be liable ambayo yako kwenye kifungu cha 25(1)(a) na shall be sentenced kifungu cha 15(1),”alisema.

Mshtakiwa Ogbechi alitiwa hatiani, Juni 19 na jana amesomewa adhabu yake ambapo upande wa mashtaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Batilida Mushi huku utetezi ukiwakilishwa na Wakili Nashon Nkungu.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshtakiwa licha ya  kwamba kifungu cha sheria cha 15(1) kinaamuru mshtakiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini siyo lazima, itolewe adhabu hiyo, mahakama inaweza kuamua vinginevyo kutokana na maneno yaliyopo kwenye kifungu cha 15(1)(a).

Mahakama ilisema pamoja na mshtakiwa kujitetea kwamba alifanyiwa upekuzi mara tatu na hakukutwa na kitu chochote na hivyo upande wa mashtaka ulipaswa kuleta ushahidi wa CCTV, haikuwa lazima kuwapangia upande wa mashitaka mashahidi wa kuwaleta na kwamba walikuwepo mashahidi wengine waliothibitisha mashitaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles