31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dawa za kulevya, ujauzito kikwazo cha elimu Muheza

NA OSCAR ASSENGA -MUHEZA

MATUMIZI ya dawa za kulevya, unyanyasaji wa kijinsia ikiwamo wanafunzi kupewa ujauzito, vimetajwa kuwa vikwazo vikubwa kwa elimu ya sekondari wilayani Muheza.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Muheza, Julitha Akkho, alipowasilisha taarifa ya hali ya elimu ya sekondari katika kikao cha wadau wa elimu.

Pia alisema utoro wa rejareja umesababisha wanafunzi wengi kukosa masomo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani hapa tofauti na miaka ya nyuma.

“Sisi tunakumbuka wakati wa miaka ya nyuma tulikuwa kinara kwenye suala la elimu, lakini sasa tunashuka na kubwa ni changamoto zinazotukabili kwa sasa, likiwemo la mimba na unyanyasaji wa kijinsia,” alisema.

Pia alisema tatizo jingine linalosababisha kuwapo kwa hali hiyo inatokana na mila na desturi potofu kwa jamii wilayani hapa.

Akizungumzia tatizo la ujauzito, alisema hali hiyo si ya kuridhisha kutokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaopata mimba kwa shule za sekondari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles