25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dawa za kulevya ndiyo chanzo kikuu cha mimba shule za Serikali wilayani Muheza

OSCAR ASSENGA, MUHEZA.

MATUMIZI ya dawa za kulevya na unanyasaji wa kijinsia ikiwemo wanafunzi kupewa ujauzito vimetajwa kuwa vikwazo vikubwa kwa shule za Serikali wilayani Muheza.

Hayo yamesemwa leo Aprili 6 na Afisa Elimu Sekondari wilaya hiyo, Julitha Akkho wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya elimu kwenye kikao cha wadau kilichofanyika mjini humo.
Amesema licha ya ujauzito pia utoro nao ni kikwazo kikubwa kinachopelekea wanafunzi wengi kukosa masomo ndiyo maana kiwango cha elimu wilayani humo kinashuka.

“Ndugu zangu sisi wilaya ya Muheza miaka ya nyuma tulikuwa kinara kwenye elimu lakini sasa tunashuka na kubwa ni changamoto zinazotukabili kwa sasa likiwemo la Mimba na unyanyasaji wa kijinsia,” amesema Afisa Elimu huyo.

Akkho amesema kwa takwimu zinaonyesha kwamba kuna ongezeko la wanafunzi wanaopata mimba katika wilaya hiyo kutoka mimba 24 kwa mwaka 2017 hadi mimba 35 kwa mwaka 2018.

Ameongeza kwamba hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2019 kuna mimba nne zimegundulika na utoro umepungua kwa mwaka 2017 ambapo wanafunzi 332 walitoroka na mwaka mwaka jana walipatikana watoto 220 waliokuwa wakitoroka shule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles