30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dawa ya wanafunzi hewa yaja

John Nchimbi
John Nchimbi

JOHANES RESPICHIUS, Dar es Salaam

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA)limeandaa mfumo mpya wa kutunza taarifa za wanafunzi kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.

Kupitia mfumo huo, mwanafunzi atapewa namba maalumu atakayoitumia kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita kuondoa tatizo la wanafunzi hewa.

Hayo yalisemwa na Ofisa Habari wa Baraza hilo, John Nchimbi alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema mfumo huo utarahisisha utaratibu kuhamisha mwanafunzi kutoka shule moja hadi nyingine  kubaini wanafunzi walioacha masomo na wanaoendelea kama njia ya kuondoa tatizo la wanafunzi hewa.

“Mfumo huu utasaidia katika uandikishaji wa wanafunzi wote wa shule za msingi kwa sababu  utatoa namba maalum ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi mbalimbali za mafunzo hususan zinazosimamiwa na NECTA.

“Pia mfumo utasaidia uandaaji na utoaji wa takwimu za wanafunzi katika ya shule, wilaya, mkoa hadi taifa na ufuatiliaji wa taarifa za matokeo ya kila mwanafunzi kuhakikisha wadau wa elimu wanapata ufahamu wa kutosha kuhusu ufundishaji na ujifunzaji,” alisema Nchimbi.

Alisema baraza hilo tayari limeshaufanyia majaribio mfumo huo katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na ifikapo Desemba, mwaka huu utaimarishwa ili Januari hadi Mei, 2017 utumiwe katika mikoa yote kusajili wanafunzi wa shule za misingi.

Alisema mfumo ni wa kisasa ambao utamaliza matatizo ya muda mrefu ambayo yanaisababishia hasara kubwa Serikali katika uendeshaji wa shule.
“Huu ni mfumo wa kwanza kutumia ndani ya nchi yetu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles