24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DAWA YA KUPUNGUZA HIV YATOA MATUMAINI

CARDIFF, WALES

JARIBIO la dawa ambayo inapunguza viwango vya maambukizi ya HIV limeleta matumaini mapya kulingana na takwimu mpya kutoka vituo vya afya vinavyotoa dawa hiyo ya Pre-Exposure Prophylaxis (Prep) mnamo mwezi Julai mwaka uliopita nchini Wales.

Taarifa zinasema kuwa, majaribio ya mwaka wa kwanza takribani watu 559 waliopo katika hatari ya maambukizi walitumia dawa hiyo ambayo imeelezewa kuleta matumaini ya kinga ya HIV, ambapo kati yao hakuna aliyepatikana na virusi vyake.

Kumekuwa na malalamiko kwa magonjwa ya zinaa miongoni mwa wale wanaoshiriki katika majaribio ya dawa hiyo, ambayo wanasayansi wamegundua, inaweza kuwalinda watu waliopo katika hatari ya kupata maambukizi iwapo itatumiwa kila siku.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza, mgonjwa mmoja aliyefahamika kwa jina la Phil, alianza kutumia dawa hiyo baada ya kutoka katika uhusiano wa muda mrefu na kuona kwamba itakuwa njia nzuri ya kuchukua tahadhari.

“Inaondoa wasiwasi wa mtu kuambukizwa virusi vya HIV. Inakupatia fursa ya kushiriki tendo la ngono bila wasiwasi,” alisema Phil alipozungumza na Redio BBC nchini Wales.

Takriban watu 150 hupatikana na ugonjwa wa HIV nchini Wales kila mwaka, nusu ya idadi hiyo ikiwa maambukizi ya ngono kati ya wanaume.

Utafiti huo wa miaka mitatu wa dawa za Prep ama Truvada, uliofanywa nchini Wales ulitangazwa mwaka uliopita na Waziri wa Afya, Vaughan Gething.

Prep ni dawa inayolinda seli katika mwili na kuharibu virusi ili kuvizuia kusambaa iwapo vitaingia mwilini. Ikitumiwa kila siku imeonekana kupunguza hatari ya maambukizi kwa asilimia 86

Kwa sasa dawa hiyo inatumika zaidi katika nchi za Marekani, Canada, Australia na Ufaransa ili kulinda watu waliopo katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya HIV. Agosti 2017 ilitangazwa kwamba dawa hiyo itapatikana kwa wagonjwa waliopo Uingereza, ikiwa ni miongoni mwa majaribio.

Dk. Olwen Williams, Rais wa Muungano wa Afya ya ngono na HIV alisema kwamba licha ya ufanisi huo, ni muhimu kutumia mipira ya kondomu unaposhiriki ngono.

“Kile tulichogundua wakati tukijadili Prep na watu binafsi ni kwamba mawazo yao, maumbile yao na vile wanavyofurahia ngono kuimeimarika,” anasema Dk. Williams.

Nchini Wales, dawa hiyo inapatikana kwa mtu yeyote anayehisi yupo katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV, hususan watu ambao hushiriki tendo la ngono lisilo salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles