23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Davido atuma salamu Kenya

NAIROBI, KENYAMSHINDI wa tuzo ya Black Entertainment Television (B.E.T) nchini Marekani, David Adeleke maarufu kwa jina la Davido kutoka nchini Nigeria, ametuma salamu nchini Kenya kuelekea shoo yake ya 30 Billion World Tour Concert.

Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika Novemba 24 kwenye ukumbi wa Uhuru Gardens, hivyo msanii huyo amedai atahakikisha anamaliza kiu za mashabiki wake nchini humo.

Davido aliita ziara hiyo jina la 30 Billion World Tour ni kutokana na wimbo wake wa ‘IF’ kufanya vizuri tangu mwaka 2017, hivyo alipanga ziara hiyo ifanyike katika nchi 30.

“Watu wangu wa Kenya burudani inakuja, mashabiki wakae tayari kwa kumaliza kiu zao, tutakuwa pamoja Novemba 24,” aliandika Davido kwenye ukurasa wake wa Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles