22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

DAVID DE GEA AIWEKA SOKONI NYUMBA YAKE

MANCHESTER, ENGLAND


MLINDA mlango wa klabu ya Manchester United, David De Gea, ametangaza kuiuza nyumba yake iliyopo jijini Manchester, kwa kitita cha pauni milioni 3.85 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 8 za Tanzania.

Tangazo la biashara hiyo ya nyumba imewashtua mashabiki wengi wa Manchester na kuwafanya waamini kuwa kipa huyo anatarajia kuondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid wakati wa uhamisho wa wachezaji kipindi cha kiangazi, hata hivyo klabu hiyo ilianza kumwinda mchezaji huyo tangu Januari mwaka huu.

Kipa huyo raia wa nchini Hispania, alijiunga na Manchester United akitokea Atletico Madrid mwaka 2011, lakini anadaiwa kutaka kurudi nyumbani.

Nyumba ambayo ameiweka sokoni ina jumla ya vyumba vitano vya kulala, sehemu ya kuogelea (swimming pool), uwanja wa tenisi, sehemu ya Sinema pamoja na vitu vingine vingi. Lakini kipa huyo amekanusha kuwa anataka kuuza nyumba hiyo ili aweze kuondoka Manchester United.

“Hakuna mtu ambaye anajua maisha yake ya baadaye, lakini kwa sasa naweza kusema ninafurahia maisha ya hapa Manchester United, ni klabu kubwa duniani yenye wachezaji wenye majina makubwa, pia ninafurahia kucheza soka nchini England.

“Sijazungumzia suala lolote juu ya kuondoka katika klabu hii, kikubwa ninachokiangalia ni jinsi gani nitaweza kuisaidia timu hii kufanya vizuri katika michezo mbalimbali na siwezi kusema kama nataka kuondoka kwa sasa,” alisema De Gea.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles