22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

DataVision yategua fumbo utunzaji taarifa

Teddy Qirtu
Teddy Qirtu

Na Mwandishi Wetu, Pwani

KAMPUNI ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ya DataVision International (DVI) wiki iliyopita, iliendesha semina kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Magharibi, Usharika wa Tumbi, Kibaha, Pwani, yenye kulenga kutoa ufahamu wa umuhimu wa kuweka taarifa na kumbukumbu.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Meneja Biashara na Uhusiano wa kampuni hiyo, Teddy Qirtu alisema maendeleo katika teknolojia ya sasa yamesaidia taasisi kubwa kama Kanisa kubadili mifumo ya uendeshaji.

Alisema viongozi wa kanisa wakiwa na taarifa za kutosha kuhusiana na waumini wao, vifaa na mali nyingine zilizo chini ya usimamizi wao, wanakuwa na nguvu ya kutenda mambo makubwa kwa sababu wana uwezo wa kuhoji au kutoa majibu sahihi wakitumia taarifa walizo nazo.

“Taarifa zote hizi humsaidia mchungaji kufanya uamuzi sahihi inapohitajika. Kuna pia utaratibu wa kutunza kumbukumbu za sadaka na matumizi. Itakuwa rahisi hata kubaini vipawa vya waumini wake vinapohitajika.

Akinukuu mfano wa kwenye maandiko ya Biblia, alisema “hata Baba yetu Adam alipotumwa na Mungu kuja duniani ilikuwa ishara ya ajira ya kwanza kwa mwanadamu. Kwa sababu alipotakiwa kutoa taarifa ya wanyama, mimea na viumbe vingine alivyoagizwa kuvisimamia ni lazima alikuwa na namna ya kutunza kumbukumbu ili akienda mbele ya Mungu wake aweze kutoa taarifa sahihi.

Kiongozi wa Jimbo la Magharibi Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Jacob Mwangomola akitoa neno la shukurani alisema mambo ya utunzaji takwimu yapo katika Biblia kwa sababu Mungu alikuwa na watumishi wake ambao alitaka wampelekee taarifa sahihi.

“Utaratibu huu utatusaidia kuondokana na taarifa za kufikirika. Tupo kwenye ulimwengu unaotembea nasi, hatuna budi kutembea kwa sababu huu si wakati wa makaratasi makubwa ya kutunzia kumbukumbu kidogo. Tunataka kitu kidogo kitakachotunza kumbukumbu kubwa,” alisema na kusisitiza:

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles