30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DAS Newala ataka misingi ya Siku ya Wanawake Duniani izingatiwe

Bethsheba Wambura

Wanawake nchini wametakiwa  kusherehekeea Siku ya Wanawake Duniani kwa kuzingatia chanzo cha sherehe hizo ambazo lengo lake ni kutetea haki zao za msingi za ambazo walikuwa wakizikosa kama kushiriki katika shughuli za kiuchumi, kiutamaduni  na kisiasa.

Siku ya Wanawake duniani  huadhimishwa Machi 8,  kila mwaka ambapo wanawake wanatambuliwa kwa mchango wa mafanikio yao bila kujali mipaka ya kitaifa, rangi, lugha, utamaduni, uchumi wala siasa.

Hayo yamesemwa  Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala, Daniel Zenda leo Ijumaa Machi 8, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Aziza Mangosongo,  katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kiwilaya yameadhimishwa katika kijiji cha Kitangari na  kauli mbiu ya mwaka huu ‘Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu’.

“ Nasisitiza juu ya jamii kubadili fikra hasi juu ya wanawake ambazo zimekuwa ni vyanzo vya kuwanyima wanawake katika maendeleo ya jamii, kila siku ingekuwa siku ya wanawake duniani laiti kama pangekuwa na mtizamo sahihi wa kijamii.

“Tunaposheherekea siku hiii ni muhimu kuwa na maneno hayo hapo juu kichwani mwetu, tuache utamaduni wa kusheherekea kwa vile ni ratiba au kwasababu wengine wanafanya hivyo, tusheherekee tukitafakari chanzo cha sherehe zenyewe cha mapambano haya ambayo lengo lake kubwa ni kutetea haki za wanawake,”amesema.

Aidha Katibu Tawala huyo alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa Newala kutumia fursa za kipindi hiki cha mvua kulima mazao ya chakula ili kuepusha kukumbwa na baa la njaa hususani katika wilaya hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles