29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Daraja lililojengwa chini ya maji Norway  

Na YASSIN ISSAH, DAR ES SALAAM

KADIRI siku zinavyozidi kwenda ndivyo ugunduzi wa vitu mbalimbali unavyozidi kukua hasa katika saula la teknolojia.

Kila kukicha wanasayansi wamekuwa wakigundua njia mbalimbali za kuweza kurahisisha mambo ili yaweze kufanyika kwa wepesi na kwa wakati sahihi ikilinganishwa na zama za hapo awali.

Matumizi ya sayansi na teknolojia katika sekta mbalimbali za maendeleo ni muhimu ili kuliwezesha taifa letu lisonge mbele.

Ukuaji wa teknolojia katika nchi za Afrika, Kusini

mwa Jangwa la Sahara ni hatua ya kutia moyo na ni jambo la muhimu licha ya changamoto kubwa ya kuyafanya mafanikio haya yawe stahimilivu kwa siku za mbeleni.

Ni changamoto kwa baadhi ya nchi za Afrika ambazo bado ziko nyuma sana katika ukuaji wa maendeleo kiteknolojia na kupanda kwa bei ya nishati na malighafi za kuzalishia vitu mbalimbali.

Katika ulimwengu wa teknolojia, ufunguo wa mafanikio ya kiuchumi unategemea sana uwezo wa nchi kupata na kutumia ujuzi kwa ufanisi

na kwa faida katika sekta za kipaumbele na ambazo zinaweza kukua kiuchumi.

Uwezo wa kupata na kuutumia ujuzi kikamilifu kuiboresha ili kupata utaalamu wa hali ya juu ambao utaziwezesha nchi za Afrika hususan Tanzania kupiga hatua katika teknolojia.

Wengi tumezoea kuona madaraja yakijengwa sehemu za kawaida kwa ajili ya waenda kwa miguu kuvuka kwa urahisi ili wasigongwe na magari au pikipiki.

Ingawa madaraja hayo wakati mwingine huwa hayajengwi kwa kiwango kilicho bora kwa usalama wa magari yenye uzito mkubwa pindi yanapovuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Unaweza ukawa umeshawahi kuona madaraja mengi na yenye mwonekano tofauti kama Daraja la Mwalimu Nyerere lililoko Kigamboni, Dar es salaam.

Daraja hilo ambalo lenye urefu wa mita 680 na upana wa mita 32 likiwa ni pamoja na njia sita za kupitisha magari, ni kati ya daraja kubwa Afrika Mashariki ambalo ujenzi wake uligharimu zaidi ya Dola za Marekani 140.

Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba Norway nayo imejenga daraja chini ya maji kwenye kivuko cha Kristiansand na Trondheim.

Katika daraja hilo magari hupita kwa saa 21 kutoka Kristiansand kuelekea Trondheim.

Daraja hilo limejengwa kwa muda wa miaka saba mpaka nane na bado wanasayansi wanafanya tafiti za kijiografia. Lina ukubwa wa futi 65 mpaka 100.

Kujengwa kwa daraja hilo kutarahisisha safari za kwenda hospitali ambazo awali watu walikuwa wakilazimika kupanda helikopta kwenda kupata matibabu katika miji mingine.

Mradi huu ikiwa utakamilika kama inavyokadiriwa na watafiti utakuwa wa kwanza duniani kwa daraja kujengwa chini ya maji na Norway itakuwa ya kwanza kugundua teknolojia hii ambayo haikuwahi kutokea sehemu yoyote duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles