28.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

DAR SOKO DOGO KUTENGENEZA MAGARI

Tphkc201112080D4

Na Joseph Lino,

SOKO la magari nchini Tanzania bado ni dogo kuvutia uwekezaji katika kiwanda cha kutengeneza magari kwa maelezo ya taasisi ya masoko ya Marekani ya Frost & Sullivan iliyokodiwa na Toyota Tanzania kufanya utafiti wa soko.

Tanzania huuza takribani magari madogo mapya 4,000, Frost & Sullivan inasema kuwa hilo ni soko dogo la magari na hivyo haliwezi kuvutia mwekezaji makini na hali ni hiyo kwa nchi nyingi za Afrika.

“Soko la ndani halina mazingira ya kujenga kiwanda na mazingira ya hapa ni kuuza nje, nchi za Afrika ambazo hutengeneza magari zinahitaji soko kubwa la kuuza nje hata Afrika Kusini,” anasema, Samantha James Meneja wa Mawasiliano.

Matumizi ya magari

“Viwango vya matumizi ya magari inakadiriwa kuwa takribani magari saba kwa kila watu 1,000 ambayo magari yake mengi ni ‘mitumba’.

Lakini uchumi si jiwe kwani kiwango hiki kinatarajia kupanda kwa kulingana na ukuwaji wa uchumi na kuongezeka kwa kipato na miundombinu ambayo itachochea matumizi ya Watanzania na hasa baada ya kuchanua uchumi wa gesi asilia,” aliongeza Ryan Bax, mchambuzi wa magari wa Frost & Sullivan Africa.

Anasema licha ya kuagiza magari mengi yaliyotumika kiwango cha wastani wa magari bado kipo chini Afrika kwa makadirio ya magari 44 kwa kila wakazi 1,000.

Anasema mauzo ya magari mapya Afrika bado ni kidogo ukilinganisha na mabara mengine, ikiwa na mauzo ya takribani milioni 1.55 kwa takwimu za mwaka 2014. Kwa maelezo yake hii inawakilisha asilimia moja ya magari mapya dunia nzima ikiwa inamaanisha gari 1.36 kwa ajili ya kila wakazi 1,000.

Takwimu zinaonesha kuwa magari madogo na abiria yalifikia 4,150 kwa mwaka wa 2015 ikiwakilisha asilimia 10.3 kwenye ukuwaji ukilinganisha na 2014.

James anasema mauzo yamekuwa yakiongezeka kwa miaka michache iliyopita kwa wastani wa magari 3,600. Anasema kinachochangia ugumu wa soko la magari mapya ni kuwepo taratibu za kodi zisizoeleweka na kodi kubwa bila sababu wakati nchi ina bandari yake yenyewe.

“Soko linatarajia kukuwa katika miaka 10 ijayo lakini itategemea hali ya uchumi, kwa sababu magari mapya mengi hununuliwa na Serikali na makampuni makubwa, magari mapya yana bei kubwa kwa Mtanzania wa kawaida. Ni uchumi wa gesi asilia tu ndiyo  itafanikisha ndoto hiyo.

Mkuu wa biashara kutoka Toyota Tanzania, Farishta Kohli, alisema gari la kawaida aina ya Corolla huuzwa kwa wastani wa dola za Marekani 26,000 ambayo ni sawa na Sh milioni 57.

Frost & Sullivan inakadiria kuwa  na wastani wa magari milioni 1.5 nchini ukilinganisha na  magari milioni 2.6 kwa Kenya ni idadi sahihi kwa nchi (critical mass). Nchi ya Ethiopia, inatafuta mwekezaji mkubwa wa viwanda vya magari katika miaka 10 au 20 ijayo ambayo kwa sasa inakadiriwa kuwa na magari mapya 500,000. Ujenzi wa treni ya kisasa umepoza mahitaji ya magari.

Kuanzishwa kwa kampeni za uwekezaji nchini Ethiopia kumevutia idadi ya makampuni ya Kichina kuanzisha viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya magari hivi karibuni na inafahamika kuwa kampuni ya Hyundai inakusudia kuanzisha shughuli zake hapo.

Hata hivyo, hali mbaya ya uchumi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo kushuka kwa bei ya mafuta, kuanguka soko la hisa kila mwaka na mabadiliko ya hali ya nchi hudidimiza uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles