Dar Mjomba wa Kenya aachia ‘Moyo’

0
723

Christopher Msekena

STAA wa gospo nchini Kenya, Dar Mjomba, amewaomba wapenzi wa muziki huo kuipokea video na wimbo wake, Moyo, aliyoiachia hivi karibuni kwenye mitandao mbalimbali.

Dar Mjomba ambaye yupo chini ya Safri Records, ameliambia MTANZANIA kuwa ndani ya wimbo, Moyo ameongelea maisha ya vijana wengi ambao huwakabidhi mioyo kwa wapenzi wao na mwisho wa siku huishia kuumizwa.

“Mpenzi anaweza akabadilika lakini ukikabidhi moyo wako kwa Mungu yeye hawezi kubadilika, huo ndio ujumbe ambao nilitaka uifikie jamii.

Naishukuru timu yangu ya Safri Records kwa kukamilisha wimbo huu na sasa video ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube na imeanza kuchezwa kwenye runinga mbalimbali hapa ndani na nje ya Kenya,” alisema Mjomba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here