24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dar kinara ukusanyaji mapato

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam, imeongoza katika kundi la Halmashauri za Majiji katika ukusanyaji wa mapato kwa kigezo cha asilimia kwa kukusanya asilimia 87 ya makisio yake ya mwaka.

Kauli hiyo ilitolewa jijini hapa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, wakati akitoa taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya tatu (Julai- Machi, 2019) kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Jafo alisema uchambuzi umefanyika kwa kulinganisha makisio ya mwaka wa fedha 2018-2019 hadi robo tatu (Julai-Machi, 2018) na mapato yaliyokusanywa kwa kila halmashauri na kwa jumla ya mkoa katika kipindi hicho kwa kushindanisha halmashauri moja moja, makundi ya halmashauri na kimkoa.

Jafo alisema Halmashauri ya Jiji la Tanga imekuwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 57 ya makisio yake ya mwaka.

Pia alisema Jiji la Dodoma limeongoza kwa kigezo cha pato ghafi (wingi wa mapato) kwa kukusanya Sh bilioni 50.

Alisema halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha mapato ya ndani yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya mwaka ni Mbozi asilimia 113, Geita asilimia 109, Wanging’ombe asilimia 105, Kilolo asilimia 103 na Sumbawanga asilimia 92.

Alisema halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha pato ghafi (wingi wa mapato) yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya mwaka ni Dodoma Sh bilioni 49.9, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Sh bilioni 44.8, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Sh bilioni 23.5, Halmashauri ya Temeke Sh bilioni 20.6 na Halmashauri ya Jiji la Arusha Sh bilioni 12.5.

NEWALA YA MWISHO

Jafo alisema halmashauri tano za mwisho kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya halmashauri ya mwaka ni Newala asilimia 15, Tandahimba asilimia 15, Mombo asilimia 13, Masasi asilimia 13 na Nanyamba asilimia 12.

“Halmashauri tano kwa kigezo cha pato ghafi yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ni shilingi milioni 293.7, Halmashauri ya Wilaya ya Newala shilingi milioni 268.3, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko shilingi milioni 238.6, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe shilingi milioni 177.3 na Halmashauri ya Wilaya ya Mombo shilingi milioni 170.4,” alisema.

Jafo aliitaja mikoa mitano iliyoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani yaliyokusanywa yakilinganishwa na jumla ya makisio ya halmashauri katika mikoa ni Iringa asilimia 77, Geita asilimia 73, Dar es Salaam asilimia 72, Dodoma asilimia 68 na Songwe asilimia 68.

Pia aliitaja mikoa iliyoongoza kwa kigezo cha pato ghafi yaliyokusanywa ukilinganisha na jumla ya makisio ya halmashauri ni Dar es Salaam Sh bilioni 118.4, Dodoma Sh bilioni 57.3, Mwanza Sh bilioni 22.9, Arusha Sh bilioni 22.8 na  Mbeya Sh bilioni 19.8.

Alisema mikoa mitano ya mwisho kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani ni Shinyanga asilimia 46, Katavi asilimia 43, Kigoma asilimia 42, Lindi asilimia 42 na Mtwara asilimia 26.

Aliitaja mikoa mitano ya mwisho kwa kigezo cha pato ghafi kuwa ni Manyara Sh bilioni 6.5, Lindi Sh bilioni 6.1, Rukwa Sh bilioni 5.8, Kigoma Sh bilioni 4.5 na Katavi Sh bilioni 3.8.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, imeongoza kundi la Halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha asilimia ambayo imekusanya asilimia 92 ya makisio yake kwa mwaka.

“Katika kundi hili, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya asilimia 23 ya makisio ya mwaka,” alisema Jafo.

Pia alisema Halmashauri ya Mji wa Kondoa imeongoza kundi la Halmashauri za Miji kwa kigezo cha asilimia ambayo imekusanya asilimia 92 ya makisio yake ya mwaka huku Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ikiwa ya mwisho na imekusanya asilimia 12 ya makisio ya mwaka.

Alisema Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kundi la Halmashauri za Miji  kwa kigezo cha pato ghafi ambapo imekusanya Sh bilioni 5.9 na Halmashauri ya Nanyamba imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya Sh milioni 293.9.

Jafo alisema Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imeongoza kundi la Halmashauri za Wilaya kwa kigezo cha asilimia ambayo imekusanya asilimia 113 ya makisio yake ya mwaka huku Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ikishika mkia kwa kukusanya asilimia 13 ya makisio yake kwa mwaka.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeongoza katika kundi la Halmashauri za Wilaya kwa kigezo cha pato ghafi kwa kukusanya Sh bilioni 4.6 na Halmashauri ya Wilaya ya Mombo imekuwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 170.4.

Kuhusiana na Mkoa wa Mtwara kutokufanya vizuri katika makusanyo kutokana na Serikali kununua korosho, alikiri jambo hilo limesababisha baadhi ya halmashauri za mkoa huo kukosa mapato na alidai jambo hilo wataliangalia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles