23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

DAR HATARINI KUKOSA MAKABURI

 

Na NORA DAMIAN

-DAR ES SALAAM

JIJI la Dar es Salaam liko hatarini kukosa sehemu ya kuzikia ambapo imeilazimu halmashauri ya jiji hilo kutenga Sh milioni 300 katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kununua eneo la kuzikia Kigamboni ama Chanika.

Mjadala wa sehemu za kuzikia ulitawala jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, huku wajumbe wakitaka eneo hilo linunuliwe haraka kwani sehemu nyingi za kuzikia zimejaa.

“Wako watu wanafariki hawana ndugu sisi tunahusika nao cha ajabu hatumiliki hata eneo, maeneo mengi yaliyopo ni ya halmashauri nyingine ambayo pia yamejaa. Ukienda Kinondoni kuna mtihani mkubwa ni utaratibu tu unafanyika ili aliyefariki asionekane…ikienda ile mifugo isiyokuwa na adabu hali itakuwa tete zaidi,” alisema Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mussa Kafana (CUF).

Naye Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF), alisema makaburi yaliyoko Kata za Makangarawe na Buza nayo yamejaa na kusababisha eneo la uwanja wa mpira kumegwa.

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), alishauri jukumu la kutafuta maeneo ya kuzikia lifanywe pia na halmashauri zingine na si kuliachia jiji peke yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles