Na Mwandishi, Dar es Salaam
RAIS Dk. John Magufuli, amemteua Gabriel Daqarro kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Arusha.
Daqarro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Uteuzi huo wa Daqarro umeanza mara moja.
Taarifa ya kuteuliwa Gambo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kupitia taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari.
Katika taarifa hiyo, Waziri Mkuu alisema Rais Dk. John Magufuli, amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Majaliwa alisema Gambo anachukua nafasi hiyo baada ya Felix Ntibenda uteuzi wake kutenguliwa.
“Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine. Kabla ya uteuzi huo, Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha,” ilieleza taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu.