25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Dante: Waleteni hao Mtibwa Sugar

Theresia Gaspeer -Dar es salaam

BEKI wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’, amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Uhuru,  Dar es Salaam.

Yanga itakutana na Mtibwa Sugar, ikitoka kupata ushindi wa mabao wa mabao 3-1 dhidi ya Singida United, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Liti Singida.

Yanga na Mtibwa mara ya mwisho zilikutana katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika Januari mwaka huu visiwani Zanzibar.

Katika mchezo huo wa hatua ya nufu fainali, Yanga ililala mikwaju ya  penalti 4-2, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Dante alisema wanaendelea kujifua vikali kwa ajili ya mchezo huo, wakitambua kuwa pointi tatu ni muhimu kwao.

“Tunahitaji kupata matokeo katika mechi zetu zinazotukabili mbele yetu, kwani tusipokuwa makini tunaweza tukapoteza na ukizingatia sisi ni moja ya timu ambayo tunatazamia ubingwa,” alisema.

Alisema watakuwa makini na kucheza kwa ushirikiano ili waweze kuwazidi mbinu wapinzani wao na kutoka kifua mbele katika mchezo huo.

Dante alisema timu hizo zikikutana mchezo unakuwa na ushindani mkubwa hivyo safari hii hawatakubali wafungwe tena na Mtibwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles