24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DANADANA YA LOWASSA POLISI YAENDELEA 

PATRICIA KIMELEMETA Na ABDALLAH NG’ANZI


 

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa jana kwa mara nyingine, alikwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es Salaam kuhojiwa akidaiwa kutoa lugha ya uchochezi.

Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  alikwenda polisi ikiwa ni mara ya nne.

Lowassa aliwasili katika Ofisi za Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), saa 3 :00 asubuhi kama alivyotakiwa na kuondoka katika eneo hilo saa 3:15 baada ya kumaliza mahojiano hayo.

Akizungumza nje ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Wakili wa Lowassa, Peter Kibatala alisema   kiongozi huyo alikwenda kwa kuitikia wito wa DCI.

“Ni mara ya nne Lowassa ameendelea kuitikia wito wa afande DCI wa kumtaka kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

“Tumefika hapa saa 3 asubuhi lakini tumeambiwa upelelezi bado haujakamilika, tuondoke hadi Agosti 14 mwaka huu,”alisema Kibatala.

Kibatala alisema dhamana ya Lowassa inaendelea na ametakiwa kurudi kituoni Agosti 14 kwa mahojiano mengine.

Kwa mara ya kwanza Lowassa aliitwa kwa DCI ili kuhojiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa alitoa lugha za uchochezi kwa masheikh waliohudhuria hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), Juni 25 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles