31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DALILI ZA KUMGUNDUA MPENZI MKOROFI, MGOMVI

DALILI hizi zitakupa tahadhari mapema mara utakapoziona zinajitokeza mara kwa mara katika mahusiano yenu.

Kusudi la makala hii ni kuwasadia wale wenye matarajio ya kuingia katika mahusiano ya kuishi pamoja kwa sababu wengi wamekuwa vipofu katika kuona baadhi ya dalili mbaya zinazoonekana katika hatua za mwanzoni wakati wa mahusiano na mara wanapoendelea mbele na kufanya maamuzi mazito hususani maamuzi ya kuamua kuoana au kuishi pamoja.

Mabadiliko makubwa yanaanza kutokea na hali hiyo huleta misuguano na maumivu baina ya wapenzi, na mbaya zaidi wengine hushindwa kabisa kuendelea na mahusiano hivyo kuamua kulivunja penzi lao.

Yatupasa wote tuliopo katika mahusiano, kabla ya kuendelea na kufanya maamuzi fulani tuwe tunatazama pia dalili za hatari. Kwa upande mkubwa dalili hizi zimeegemea kuwasaidia zaidi jinsia ya kike kujua au kuwafahamu wanaume.

Hii ni kwa sababu wanawake ndio ambao wamekuwa wakionesha kuumizwa zaidi na kukatishwa tamaa na mabadiliko ya tabia za wanaume mara wanapozama katika dimbwi la mapenzi.

Ingawa wapo pia wanaume wanaoumizwa kutokana na mabadiliko ya tabia za wapenzi wao, na wao pia waweze kuzitazama dalili hizi.

Dalili: 

  • Mpenzi wako anakuwa na wivu sana kwa ule muda unaotumia kuwa na wafanyakazi wenzako, marafiki na hata ndugu zako, ingawa sio kwamba anataka muda huo awe na wewe.
  • Anakuwa na tabia za kukuudhi na kukutawala, ataangalia sana kutoka na kuingia kwako, nyendo zako na hata matumizi yako ya fedha, na kama ukimuuliza kwanini anafanya hivyo atajiteteta kuwa anakusaidia kufanya maamuzi sahihi.
  • Taratibu anakutenga na wote waliokaribu na wewe, pia anajaribu kukutenga na wale wanaoonekana kuwa msaada kwako kama vile wale unaowasiliana nao kwa simu, wafanyakazi wenzako na hata ndugu zako wa karibu.
  • Huwa na tabia ya kuwalaumu sana wengine kwa matatizo anayoyapata yeye. Mfano anapokosa kazi, anaposhindwa shuleni, anapokosa pesa nk. Kila kitu ni kosa la mtumwingine na sio yeye.
  • Hukasirishwa na kuudhiwa na vitu vidogo vidogo na vya kawaida katika maisha ya kila siku, mfano akiambiwa afanye kazi zaidi ya muda wa ofisi, akiombwa amwangalie mtoto, anapopingwa katika kitu kidogo nk.
  • Anakuwa na tabia za kikatili kwa wanyama wafugwao “pets” na hata kwa watoto. Haumizwi pale anapoona maumivu au kuteseka kwa kiumbe kingine. Anaweza kujiona anacheza au anatania bila kujua anamuumiza mtoto au mnyama.
  • Ni wenyetabia ya mabavu hususani katika tendo la ndoa, hawatojali hisia zako, umelala usingizini au unaumwa, bali hujali zaidi kuzitimiza haja zao.
  • Ni wenye maneno makali yakuumiza na ya kushusha hadhi, huweza kukuamsha usingizini ili akutukane au kukugombeza. Akianza malumbano hakupi upenyo wa kwenda kulala, anaweza kulalama usiku mzima.
  • Sio watu wakutabirika, ni watu wenye hisia za kubadilika badilika, mara muda huu anafuraha na kuonyesha mapenzi, mara ghafla kakasirika na kutaka kuadhibu mtu.
  1. Anaweza akawa na historia ya tabia za kikorofi na kigomvi, labda amewahi kuwa na matukio ya kuwapiga marafiki zake, akijitetea kuwa alipitiwa tu na hasira.
  2. Ni mwenye vitisho na tabia za kuashiria fujo, mfano kupenda kutishia akisema “nitakuzaba vibao” “nitakuuwa ‘I will kill you if….”, “nitakuvunja shingo”, “ntakufanyia kitumbaya” n.k.
  3. Mwenye tabia ya kupiga au kugonga vitu kwa hasira, kuvunja vitu vyako, kukurushia vitu wewe au watoto kwa hasira.
  4. Hutumia nguvu anaposisitiza hoja yake, mfano, kukushika nguo au kukukandamiza ukutani na mara nyingine kukusukuma.
  • Tafiti zimegundua kwamba, kama mtu anaonyesha tabia za fujo na kijeuri wakati wa urafiki au uchumba kunauwezekano mkubwa wa kuwa mtu wa hatari zaidi mara atakapoingia kwenye ndoa. Kamwe usijidanganye na kujifariji kwamba hivyo vijitabia anavyovionyesha sasa eti atabadilika tu mara mkioana. Sahau.

Kumbuka ; fujo huzaa fujo, na ujeuri huzaa ugomvi na kwa haraka vyote hivi huua mapenzi kwa wale wanaopendana.

Na: Chris Mauki

Counselor and Social Psychologist

University of Dar es Salaam

[email protected]

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles