21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

DALEY BLIND AFURAHIA KUJIUNGA AJAX

AMSTERDAM, UHOLANZI

ALIYEKUWA kiungo mkabaji wa Manchester United, Daley Blind, amesema anafurahi kurudi katika klabu yake ya zamani ya Ajax, baada ya kuitumikia United kwa kipindi cha miaka minne.

Klabu ya Ajax imemsainisha tena mchezaji huyo kwa mkataba wa pauni milioni 14, lakini inadaiwa kiasi hicho cha fedha kinaweza kuongezeka hadi kufikia milioni 18.

Ajax walitumia ukurasa wao wa Twitter na kutuma video ikimuonesha mchezaji huyo pamoja na ujumbe ambao unasema: “Daley amerudi nyumbani, tayari amefika nyumbani,” waliandika Ajax.

Hata hivyo, mchezaji huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuelezea jinsi alivyo na furaha kurudi katika klabu yake ya zamani.

“Kwanza ninaanza na kushukuru kuwa miongoni mwa wachezaji wa Man United kwa kipindi cha miaka minne, nilikuwa kama sehemu ya familia yangu.

“Kupata nafasi ya kucheza kwenye klabu kubwa kama hiyo ni historia, nimekuwa hapo kwa miaka minne na kufanikiwa kupata mataji manne, napenda kuwashukuru wote ikiwa pamoja na makocha, idara ya huduma ya afya, wachezaji wenzangu, mashabiki na wale wote waliohusika mimi kuwa hapa.

“Kwa sasa naweza kusema nimerudi nyumbani, nawashukuru sana kwa kunipokea na nina furaha kwa kuwa nipo nyumbani,” alisema Blind.

@@@@@@@@@

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles