22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Daladala ruksa kusimamisha wanafunzi watano

Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameruhusu makondakta wa daladala kusimamisha wanafunzi wasiozidi wanne.

Alitoa agizo hilo jana wakati akipokea vifaa tiba vya ujenzi vilivyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) vyenye thamani ya Sh milioni 120.

“Kutokana na agizo la Wizara ya Afya la kuagiza daladala kutosimamisha abiria, ikiwa ni njia ya kuepuka  maambukizi ya corona, daladala zimekuwa zikiwabagua wanafunzi.

“Sasa nataka makondakta wa daladala zote wawaruhusu wanafunzi wapande kuanzia wanne hadi watano wasimame ili wafike shule haraka kuwahi masomo na kurudi nyumbani.

“Madereva wa daladala hawatakiwi kuwaacha wanafunzi kwa kuwa ni ‘level seat’, na matrafki waacheni madereva wawapandishe wanafunzi wanne au watano wawahi masomo na kurudi nyumbani, ukimkuta na wanafunzi ni halali yake mwache,” alisema Makonda.

Aidha aliwasihi makondakta kutowasimamisha watu wasiokuwa wanafunzi kwani katazo bado lipo vilevile hadi Wizara ya Afya ikitoa tamko.

Pia Makonda alisema bado bodaboda na bajaji wanaruhusiwa kufika mjini na kuchukua abiria hadi hapo atakapotoa agizo jingine.

“Bodaboda na bajaji mnatakiwa kuendelea kuingia mjini kutafuta pesa kwa ajili ya kujipatia kipato cha kulisha familia zenu.

“Mnaowakamata bodaboda na bajaji, niwaambie hakuna mkuu wa mkoa mwingine ila ni mimi, bado nawaruhusu kuingia mjini, kuna watu wameanza juzi kuwakamata bodaboda na bajaji wakiingia mjini, mkiendelea kuwakamata nitawakamata wao wenyewe,” alisema Makonda.

Aidha Makonda alisema wanaendelea na ujenzi wa ofisi za walimu na kuboresha huduma za afya kwa kutoa vifaa na wahudumu wa kutosha katika hospitali ambazo zimejengwa kwa maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Augustine Witonde alisema wanaendelea kutoa msaada ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

“Tumetoa mashine mbili za Ultrasound kubwa na ndogo, pia milango ya aluminum 37na madirisha 27, milango ya magril 8 na madirisha 53, vyote hivyo vimetengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),” alisema Witonde.

Alisema vifaa vyote hivyo vinagharimu Sh milioni 120 na kuwataka wananchi waendelee kutumia bandari yao na rasilimali zake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, alisema TPA hawapo mbali na wilaya yake kwakuwa mwaka jana walitoa mashuka na round table kwa wajawazito kujifungulia.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles