23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Daktari: Msongo husababisha kuzaa mtoto mlemavu wa akili

Na Amina Omari -Tanga

MSONGO wa mawazo wakati wa ujauzito ni miongoni mwa sababu za kuzaa mtoto mwenye ulemavu wa akili.

Hayo yameelezwa na mtaalamu wa magonjwa ya akili, Mwanaidi Hamza katika kituo cha matibabu ya magonjwa hayo kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Bombo mkoani Tanga.

Alisema msongo wa mawazo husababisha athari kwa mjamzito, lakini athari kubwa huenda kwa mtoto na wakati mwingine husababisha udumavu.

“Kwa sasa kuna kesi nyingi za watoto kushindwa kuendana na hatua za ukuaji wa watoto kunakotokana na athari za msongo wa mawazo,” alisema Mwanaidi.

Alisema unaweza kukuta mtoto ana miezi sita, lakini bado hata kunyanyua mkono hawezi.

“Hiyo inatokana na athari za msongo wa mawazo,” alisema Mwanaidi.

Alisema licha ya mihangaiko ya maisha, lazima jamii imwepushe mjamzito matatizo yatakayomsababishia msongo wa mawazo ili aweze kuzaa mtoto mwenye afya bora.

Mwanaidi alisema tatizo la kuzaa watoto wenye ulemavu linaweza kwisha kabisa kwenye jamii iwapo wazazi watazingatia lishe bora.

“Ni elimu pekee ndiyo itakayoweza kuleta mabadiliko kwa jamii na kuachana na mila potofu ambazo zimepitwa na wakati,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles