25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Daktari mbaroni kwa wizi wa dawa

Na Gurian Adolf-KATAVI

JESHI la Polisi mkoani Katavi, inamshikilia Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Inyonga wilayani Mpanda, Calvin Mnaso (37), tuhuma za kuiba dawa za binadamu pamoja vifaa tiba katika kituo hicho.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga alisema kuwa mtuhumiwa huyo  alikamatwa Desemba 19, baada ya polisi kupata taarifa za wizi katika kituo hicho.

Alisema baada ya taarifa hizo, polisi walianza kupekua katika nyumba za baadhi ya watu waliohisiwa kuhusika na wizi huo wakiwemo baadhi ya watumishi wa kituo hicho cha afya.

Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa, walipofika nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata mabox matano ya dawa mbalimbali za binadamu, vifaa vya kupima maradhi ya binadamu, vifaa vya kufanyia oparesheni na tohara, godoro moja pamoja na sindano ambazo zote ni mali ya serikali.

Baada ya kukamata vitu hivyo mtuhumiwa huyo alishikiliwa na polisi kwa  upelelezi pindi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles