22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Daktari bingwa mifupa, uti wa mgongo kuwasili

Na Mwandishi Wetu

MTAALAMU wa maradhi ya mgongo na mifupa kutoka India, anatarajiwa kuwasili nchini wiki hii ambapo watawafanyia uchunguzi watu mbalimbali wenye maradhi hayo.

Taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Regency, Dar es Salaam jana, ilisema Dk. Viral Shah ambaye amebobea kwenye maradhi ya mgongo .

Alisema mtaalamu huyo anatoka taasisi kubwa ya tiba ya Shalby, Ahmedabad- Gujarat  ya nchini India ambayo ni moja ya hospitali kubwa barani Asia na atafanya uchunguzi huo kwa siku mbili kuanzia tarehe 19 na 20 wiki hii.

“Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kuhudumiwa na wataalamu bingwa wa maradhi ya mgongo, magoti na nyonga hivyo tunawaomba watumie fursa hii kuwaona wataalamu hawa,” alisema na kuongeza kuwa wale wanaotaka kuwaona wataalamu hao waje na x ray zao hivi karibuni na ripoti za madaktari walikokuwa wakitibiwa.

“Watu 200 wa kwanza ndio watakaopata fursa ya kuwaona wataalamu hawa hivyo tunawahamasisha wenye matatizo kama hayo waende kuwaona wataalamu hao hospitali ya Regency ili wapate tiba na ushauri,” ilisema.

Ilisema watakaofika watapata fursa ya kupata ushauri wa maumivu ya shingo, taratibu za upasuaji, maumivu ya mgongo na matatizo ya uti wa mgongo.

Ilisema Dk. Viral Shah ambaye ni mtaalamu wa migongo atafanya kliniki yake katika hospitali ya Regency,Dar es Salaam Desemba 19 na 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles