25.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Daktari atuhumiwa kuwapa sumu wagonjwa

BESANCON, UFARANSA

DAKTARI wa binadamu, Frederic Pechier raia wa Ufaransa ambaye tayari anachunguzwa kwa kuwapa sumu wagonjwa saba, ameshtakiwa kwa kuwapa sumu watu wengine 17 katika kliniki moja ya Mashariki mwa Ufaransa.

Pechier mwenye umri wa miaka 47, sasa anakabiliwa na mashtaka 24, ambapo matukio tisa yalisababisha vifo, baada ya kufanya kazi kama daktari bingwa katika kliniki mbili binafsi kwenye mji wa Mashariki mwa Ufaransa wa Besancon.

Endapo atapatikana na hatia, Pechier, huenda akahukumiwa kifungo cha maisha. Wakili wake amesema Pechier aliachiwa huru bila masharti usiku wa kuamkia jana. Mwendesha mashtaka, Etienne Manteaux, alikuwa anataka daktari huyo kuwekwa kizuizini.

Pechier ambaye alishtakiwa mara ya kwanza mwaka wa 2017 kwa vifo viwili katika kesi saba za kupewa wagonjwa sumu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, alihojiwa wiki hii kuhusiana na matukio 66 yaliyoshukiwa kuwa ya mshtuko wa moyo wakati akiwafanyia upasuaji wagonjwa ambao hawakuonekana kuwa katika hatari kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles