Dakika 90 za soka zamchosha Wema Sepetu

0
1135

Wema-SepetuNA CHRISTOPHER  MSEKENA

DIVA kutoka kiwanda cha filamu za Kitanzania, Wema Sepetu, amefunguka kuwa mchezo  wa soka unamchosha kuangalia kwa kuwa unatumia muda mrefu wa dakika 90 huku wachezaji wake wakihangaika mno kutafuta bao tofauti na mpira wa kikapu.

Wema Sepetu, alilidokeza Swaggaz, kuwa mara nyingi akiwa nyumbani kwake huwa anaangalia mpira wa kikapu kwani hauchoshi na wachezaji huwa wanatumia muda mfupi kupachia mabao.

“Mpira wa miguu unanichosha, siwezi kuvumilia dakika 90 zote ziishe kwani ni muda mrefu tofauti na ilivyo kwenye Basketball, ambapo mabao yake hupatikana kirahisi na mchezo hauchukui muda mrefu,” alisema Wema Sepetu.

Aliongeza kuwa ili aangalie soka na kumaliza muda wote wa mchezo ni lazima awe na kampani yake na mara nyingi iwe laivu uwanjani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here