23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

CWT yahimiza walimu kutoa maoni kuhusu uundwaji wa bodi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kimewataka walimu nchini kuendelea kutoa maoni  kuhusiana na uanzishwaji wa Bodi ya Kitaaluma ya walimu Tanzania huku ikisisitiza msimamo wao ni  kuipinga na kuikataa bdi hiyo kwani imelenga kumkandamiza mwalimu badala ya kumsaidia.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Julai 10,2021 na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Deus Seif wakati   akifungua kongamano la walimu tarajali na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza pamoja na  kuwaaga wanafunzi walimu mwaka wa tatu lililofanyika katika kitivo cha Walimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).

Katibu Mkuu huyo amesema wakiwa Mwanza katika Mei Mosi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan aliagiza walimu washirikishwe kutoa maoni kuhusiana na Bodi ya Kitaaluma ya walimu.

Amesema wao CWT Msimamo wao ni ashirikishwe mwalimu mwenyewe ili aweze kutoa maoni kwani kila mmoja amekuwa akiwasemewa hivyo kuna haja ya kuwa na chombo kimoja ambacho kitawasemea walimu katika mambo yao.

“Kilio cha walimu kinasemwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Tamisemi,Wizara ya Fedha na Mipango,Utumishi huyu ni mtu mmoja hata katika Soka makocha sita watawezaje kuiendesha timu Sisi kama CWT tumeotoa maoni yetu uimarishwe  utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

“Uzuri CWT ina walimu kila sehemu naomba tushirikiane kutoa mawazo hivi ni kweli mwalimu anatakiwa aende mafunzo kila mwaka tena alipie kwa fedha yake ili kuboresha leseni yake tena mafunzo yenyewe yanagharama tunasema hapana katika hili,”amesema Katibu Mkuu huyo.

Katika hatua nyingine,Katibu Mkuu huyo ameoneshwa kusikitishwa na walimu ambao wamekuwa hawaaminiki wakati wa kipindi cha usimamizi wa mitihani.

“Zamani hadhi ya mwalimu ilikuwa juu kuna wakati walimu wa shule husika walikuwa wakisimamia mitihani ya mwisho katika madarasa ambayo wanayafundisha na hakukuwa na tatizo lolote,baada ya hapo kikaja kizazi cha Digital  tukaanza kuletewa mgambo,sisi sio waaminifu  ni tatizo,”amesema.

Amesema ni lazima walimu wawe waadilifu ili jamii iweze kuwakubali ambapo amedai kwa sasa hali inavyoelekea kuna siku Jeshi la wananchi litakuja kulinda mitihani jambo ambalo sio zuri kwa walimu.

“Lazima mtuje ile mitutu ambayo inaletwa sasa hivi inalinda uaminifu na tunapoenda kwa sasa Jeshi la wananchi litakuja kusimamia mitihani hatujachelewa bado tuna nafasi tunatakiwa kuwa waadilifu,amesema Katibu Mkuu.

Akizungumzia ajira za walimu alisema mwaka jana walipeleka ombi kwa Hayati, Dk.John Magufuli kuhusu ajira za walimu ambapo alilikubali na ndio ulikuwa msingi wa walimu zaidi ya nafasi 6000 za ajira zilizotolewa na serikali hivi karibuni.

Seif alisema CWT itaendelea kuwasilisha ombi hilo kila inapopata nafasi ya kukutana na kuzungumza na serikali na kushauriana katika mambo mbalimbali.

Akizungumzia jukumu la CWT la utetezi kwa walimu amesema  mpaka sasa imefanikiwa kushinda asilimia 89 ya kesi zinazohusiana na mashauri ya walimu.

“CWT imekuwa ikisimamia kesi za walimu pale mwalimu anapokuwa na shauri mahakamani linalohusu masuala ya kikazi, tunamuwekea wakili na tunaendesha kesi kuanzia mwanzo hadi mwisho ikiwa ni pamoja na kumlipa wakili atakayekuwa akisimamia kesi hiyo,”amesema

Awali akisoma risala Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSTA) Emanuel Mwangoka  amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017 chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vyanzo vya mapato na hivyo kufanya chama kujiendesha kwa michango ya wadau kikiwemo CWT.

Pia, amesema wao kama walimu tarajali wameomba wapewe elimu kuhusiana na Bodi ya walimu Tanzania ili waweze kuifahamu utendaji kazi wao na walimu watanufaikaje na Bodi hiyo.

Ameitaja changamoto nyingine kuwa ni wanachama (walimu) wanaojiendeleza be wamekuwa wakikosa haki zao kama watumishi hasa katika suala la kuzuiwa kupanda madaraja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles