30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

CWT yachangia ujenzi nyumba za walimu

GUSTAPHU HAULE

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa msaada wa fedha taslimu Sh milioni tatu kusaidia ukarabati wa miundombinu ya nyumba za walimu na baadhi ya shule zilizoathiriwa na mafuriko ya mvua kubwa zilizonyesha Wilaya za Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Msaada huo umekabidhiwa jana na Mwekahazina wa CWT Taifa, Aboubakary Alawi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Alawi alisema kuwa wameamua kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuweka mazingira mazuri ya kufundishia kwa walimu.

Alisema kuwa pamoja na kuwa CWT ni chama cha kutetea masilahi ya walimu, lakini kwa sasa wameamua kuungana kusaidia kurejesha miundombinu ya walimu ambayo imeharibiwa na mafuriko.

“Tumeguswa na hali ya taharuki iliyowapata walimu wenzetu wa Rufiji na Kibiti, tumekuja kutoa mchango wetu kwako mkuu wa mkoa,” alisema Alawi. 

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Ndikilo alishukuru na kuomba kampuni nyingine ambazo zimewekeza katika mkoa huo kuiga mfano wa CWT.

“CWT ni taasisi inayojitambua, inayoshughulika na matatizo ya wananchi na katika hili niwapongeze kwa kuunga mkono juhudi za Serikali.

“Serikali haiwezi kujenga barabara zote, nichukue fursa hii kuwaomba wadau wengine na wamiliki wa viwanda Pwani kuiga mfano huu na kusaidia changamoto zilizopo kwa wilaya zetu za Kibiti na Rufiji,” alisema Ndikilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles