27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Curry achukua tuzo ya MVP

Stephen CurryCALIFORNIA, MAREKANI

NYOTA wa mchezo wa kikapu nchini Marekani ambaye anakipiga katika timu ya Golden State Warriors, Stephen Curry, ametwaa tuzo ya MVP kwa mara ya pili mfululizo.

Nyota huyo kwa sasa anaingia kwenye rekodi ya uchezaji bora wa kikapu na kuzifuata nyayo za Michael Jordan na LeBron James.

Mchezaji huyo amepata tuzo hiyo kutokana na kupigiwa kura ambapo alifanikiwa kupata jumla ya kura 131.

“Sikutarajia kuona kitu kama hiki kikitokea, ninaamini ninachokifanya katika mchezo huu kitawapendeza vijana wa kizazi kijacho, lakini hii inatokana na kujituma uwanjani.

“Hata mimi nimefika hapa baada ya kuwaona waliotangulia wakifanya vitu ambavyo vilikuwa vinawagusa wengi, nikawa najituma kwa ajili ya kuwa kama wao,” alisema Curry.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles