23.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Cuppy Music awapa shavu Rayvanny, Rema

Na CHRISTOPHER MSEKENA

MREMBO ambaye ni Dj na mtayarishaji nyota wa muziki nchini Nigeria, Florence Otedola ‘Cuppy’, amefurahia kuwakutanisha wasanii wanaofanya vyema barani Afrika, Rayvanny na Rema katika ngoma yake mpya, Jollof On The Jet.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cuppy alisema ngoma hiyo ni mchanganyiko mzuri wa Afro Pop na Afro Beat ambao umeleta ladha na msisimko mpya kwa mashabiki wa muziki Afrika.

“Kufanya kazi kwa ushirikiano huu  wa Rayvanny na Rema wa hapa Nigeria umenitia sana moyo, ni Afro Pop iliyoboreshwa japo hatujarekodi pamoja studio lakini tumetoa ngoma kali ambayo naamini kila mmoja ataipenda hivyo naomba sapoti kutoka kwa mashabiki Afrika Mashariki,” alisema Cuppy ambaye tayari amefanya kazi na mastaa kibao akiwamo Tekno na Zlatan.

Mrembo huyo ambaye alianza kujipatia umaarufu mwaka 2014 kwenye tuzo za MTV Africa Music na mwaka uliofuata alifanya ziara yake ya ‘Cuppy Takes Africa Tour’ ambayo iliwekwa kwenye makala inayoruka Fox Life.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,437FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles