Cunningham  kavunja rekodi ya  Ogogo

0
701

anthony-ogogo-article-3BIRMINGHAM, ENGLAND

BONDIA Anthony Ogogo amepoteza rekodi yake ya kutopigwa katika mapambano ya 11, baada ya juzi kupigwa na Craig Cunningham katika pambano la uzito wa kati la kuwania mkanda wa  WBC lililofanyika katika ulingo wa   Birmingham Arena, England.

Ogogo ambaye alifanikiwa kunyakua medali mbalimbali za Olimpiki mwaka 2012, juzi alishindwa kuzuia kutodondoka kutokana na uzito wa ngumi ya kulia ya bondia Cunningham katika mzunguko wa pili wa pambano hilo.

Cunningham amepoteza pambano moja kati ya 18, alipewa  alama  20-1 ya uwezekano wa kumchapa Ogogo katika pambano hilo.

Lakini Ogogo alipambana kadiri awezavyo, hata hivyo baadaye alikubali kipigo hicho kutoka kwa Cunningham.

Cunningham alisema: “Napenda kuwa mpambanaji na hakuna kinachonitisha mbele yangu.

“Nilimchunguza kasi yake na kujipanga kabla ya siku ya pambano ili kuweza kumdhibiti kikamilifu mpinzani wangu.

Cunningham alieleza kuwa licha ya kutokuwa na rekodi nzuri ya kutosha chini wapinzani wake, amefanikiwa kufanya  hivyo kwa Ogogo.

Wakati huo huo, bondia, Sam Eggington, alimchapa makonde makali bondia, Frankie Gavin, katika pambano la kuwania mkanda wa WBC.

Eggington alifanikiwa kumdondosha chini Brummie katika mzunguko wa sita, baada ya kumvurumishia makonde mfululizo akiwa pembeni mwa kamba ya ulingo kabla ya mwamuzi kusimamisha pambano hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here