24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

CUF Maalim Seif wateua wajumbe wa bodi

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BARAZA Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wamekutana na kufanya uteuzi wa wajumbe wanane wa bodi ya wadhamini.

Hatua hiyo imekuja siku mbili baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Benhajj Masoud,  kutengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya upande ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Pamoja na hali hiyo pia Jaji Masoud alisema hata wajumbe wa upande wa Maalim Seif, nao hawatambuliki kwani wamekosa uhalali kisheria.

Taarifa iliyotolewa na CUF jana ilieleza kuwa juzi Baraza Kuu la CUF upande wa Maalim Seif, lilikutana jijini Dar es Salaam na kufanya uteuzi wa wajumbe hao.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob kama Ofisa kutoka Mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya The Trustees incorporation Act. CAP 318 RE: 2002 Section 17(1).

Pia kikao hicho kilimwalika  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia.

“Kikao kilikuwa na ajenda moja pekee ambayo ni kujaza nafasi za wajumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF, ambapo wajumbe 37 walihudhuria kati ya wajumbe wote 63 kama wangekuwepo kama walivyochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa mwaka 2014.

Na hivyo kufanya kupatikana (koramu) ya zaidi ya nusu ya wajumbe halali waliopaswa kuhudhuria kikao hicho” ilieleza taarifa hiyo.

Wanachama walioteuliwa kujaza nafasi za wajumbe wa bodi ya wadhamini ni Abdallah Khatau, Ali Mbaraka Suleiman, Yohana Mbelwa na Mohamed Nassor Mohamed.

Wengine ni Dk. Juma Ameir Muchi, Zumba Kipanduka, Mwanawetu Zarafi, Mwana Masoud Ali na Blandina Mwasabwite.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles